Chorus / Description :
Baba umenipa nafasi nyingine
Unanipenda tena bila kukoma (nafasi nyingine)
Neema yako imeniinua tena (nafasi nyingine)
Umenipa tena bila kuchoka (nafasi nyingine)
Wa neema Mungu wa neema
Wa neema neema aaah aah
Mavumbi umenivuta yote
Habari umebadili yote
Machozi umenifuta yote
Aibu umeondoa yote
Umeniita mwana niliyekuwa mtumwa
Umenisimamisha katika wingi wa neema
Na umeniketisha mahali pa juu sana
Ninaucheka wakati uliyopita
Nikiufurahia ule ujao
Ninaucheka wakati uliyopita
Nikiufurahia ule ujao
Baba umenipa nafasi nyingine
Unanipenda tena bila kukoma (nafasi nyingine)
Neema yako imeniinua tena (nafasi nyingine)
Umenipa tena bila kuchoka (nafasi nyingine)
Wa neema Mungu wa neema
Wa neema neema aaah aah
Madakari walisema sitapona tena
Walimu walisema nitafeli
Ndugu na jamaa walisema nimeshindikana
Na kumbe kwako wee waniwazia mema
Umri uliposogea walisema ndoa si fungu langu
Nilipofiwa na mpendwa walisema siwezi tena
Baada tu ya kufilisika sikuona wakuniombea
Na kumbe ndani yao walifurahi niliyopitia