Chorus / Description :
Eeh Bwana nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)
Eeh Bwana nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)
Mambo ni mengi nimepitia
Machozi ni mengi nimelia
Hata kicheko ni cha bandia
Inafunika mengi ninayopitia
Ila najua iko yako
Ya pili isiyo na haya majuto
Tena si ya ulimwengu ule uchao
Ila ni ya ulimwengu huu wa leo
Eeh Bwana nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)
Eeh Bwana nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)
Maana najua sikusudi lako niishi hapa
Maana najua si kusudi lako nikwame
Maana najua si kusudi lako niaibike
Maana najua si kusudi lako nianguke
Sasa nyosha mkono wako univushe ng'ambo ya pili
Bwana nimefika mwisho wa uwezo wangu wa akili
Nimekuja ishiya leo mazuri uliyoniahidi
Nisiyaone kwa mbali niyashike na kuyamiliki
Nivushe nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)
Eeh Bwana nivushe nivushe ng'ambo
Nivushe ng'ambo (Nivushe ng'ambo)