Joel Lwaga - Umenikubali

Chorus / Description : Bwana Umenikubali Jini Nilivyo
Umenikubali Jinis Nilivyo
Umeona Jema ndani yangu na Wala hukutazama Unyonge wangu

Umenikubali Lyrics

Kama Mungu ungetazama
Kama watu tunavyotazama
Nisingetosha kwenye mizani
Nisingekidhi masharti
Hukuangalia historia ya familia niliyotokea
Hazikukutisha zangu tabia ulilitazama lililo Jema

Umenipenda nisiyestahili
Umeniita mwanao
Niliyejidhania kuwa sifai
Umenipenda Upeo
Umebadilisha na yangu asili
Umenifanya mboni ya jicho lako

Ungehitaji walio kamili
Mimi si mmoja wao
Ulichojali wangu utayari wa kufanya utakalo
Umenikabidhi na zako siri Na kunifanya rafiki wa moyo wako

Bwana Umenikubali Jini Nilivyo
Umenikubali Jinis Nilivyo
Umeona Jema ndani yangu na Wala hukutazama Unyonge wangu


Kuna muda najiuliza Wewe ni Mungu wa namna gani
Uliyenipenda na kunikubali mtu wa namna hii
Ziko nyakati hata mimi napata shida kujikubali Iweje wewe unipende mtu wa namna hii

Umenipenda Nisiyestahili
Umeniita mwanao
Niliyejidhania kuwa sifai
Umenipenda Upeo
Umebadilisha na yangu asili
Umenifanya mboni ya jicho lako

Ungehitaji walio kamili
Mimi si mmoja wao
Ulichojali wangu utayari wa kufanya utakalo
Umenikabidhi na zako siri Na kunifanya rafiki wa moyo wako

Bwana Umenikubali Jini Nilivyo
Umenikubali Jinis Nilivyo
Umeona Jema ndani yangu na Wala hukutazama Unyonge wangu

Ahsanteee Ahsanteee Ahsantee Ahsantee maana
Umeona Jema ndani yangu hukutazama Unyonge wangu

  • Song: Umenikubali
  • Artist(s): Joel Lwaga


Share: