Chorus / Description :
Wadumu milele
Wadumu milele
Bwana Wadumu milele
Wadumu milele
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Msimamizi wa mipaka ya bahari
Utunzaye gala ya mvua
Waamua vita ya jua na mwezi
Pepo na mawimbi yakujua
Uketiye mahali pa siri
Patakatifu palipoinuka
Wautangaza mwisho mwanzoni
Hakuna usilolijua
Nani wa kulinganishwa nawe
Jehovah mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa thamani zote
Vizazi vyote
Pre-chorus
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Chorus
Wadumu milele
Wadumu milele
Bwana Wadumu milele
Wadumu milele
Wewe Bwana ni kama maji
Maji yenye kina kirefu
Kamwe hayapigi kelele
Ni kweli kuna mabwana wengi
Lakini wewe ni Bwana wa Mabwana
Ni kweli kuna miungu mingi
Lakini wewe ni Mungu wa Miungu
Siku kwako sio vipindi
Majira kwako sio ishara
Hufikiwi kwa mnara wa babeli
Jina lako ni ngome imara
Nani wa kulinganishwa nawe
Jehovah mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa zamani zote
Vizazi vyote
Pre-chorus
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Miaka kwako sio umri
Vizazi kwako si ukomo
Chorus
Wadumu milele
Wadumu milele
Bwana Wadumu milele
Wadumu milele
Outro
Say
Yeah Yeah
Yeah Yeah
Nani wa kulinganishwa nawe
Jehovah mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa milele yote Bwana