Chorus / Description :
Eeh Bwana, wanitazama
Baba, baba Mungu usiyelala
Wanitazama, wanitazama
Baba, baba Mungu usiyechoka
Mkono wako umenishika
Fimbo yako yaniongoza
Gongo lako lanifariji
Umenisitiri umenifanya hodari
Uliliona chozi langu la ndani
Ukalifuta na kunipa amani
Unyonge wangu haukukuweka mbali
Ukaniinua na kunipa dhamani
Eeh Bwana, wanitazama
Baba, baba Mungu usielala
Wanitazama, wanitazama
Baba, baba Mungu usiyechoka
Mi ni mboni yako
(Yesu wee, Yesu wee)
Jicho lako
Yesu wee, Yesu wee
Mi ni mboni yako
(Yesu wee, Yesu wee)
Jicho lako
(Yesu wee, Yesu wee)
Akili zangu Zilifika mwisho
Na kuona Mungu hunitazami taabuni
Na wanadamu
Wakapata cha kusema kuwa
Mungu wangu hayupo tena nami
Nilipoona ni mwisho
Wewe ukatangaza mwanzo
Nilipodhani ni pigo
Kumbe ni lako kusudio
Kilipozidi kilio
Wewe ukaleta kicheko
Ukadhihirisha kwa macho
Wewe ni langu kimbilio
Uliliona chozi langu la ndani
Ukalifuta na kunipa amani
Unyonge wangu haukukuweka mbali
Ukaniinua na kunipa dhamani
Eeh Bwana, wanitazama
Baba, baba Mungu usielala
Wanitazama, wanitazama
Baba, baba Mungu usiechoka
Eeh Bwana, wanitazama
Baba, baba Mungu usielala
Wanitazama, wanitazama
Baba, baba Mungu usiyechoka
Mi ni mboni yako
(Yesu wee, Yesu wee)
Jicho lako
Yesu wee, Yesu wee
Mi ni mboni yako
(Yesu wee, Yesu wee)
Jicho lako
(Yesu wee, Yesu wee)
Uliliona chozi langu la ndani
Ukalifuta na kunipa amani
Unyonge wangu haukukuweka mbali
Ukaniinua na kunipa dhamani
Eeh Bwana