Yote Mema Lyrics

Aaaaah Mema, aaah mema [x3]
Ni rahisi kukusifu 
Wakati wakati wa mazuri 
Ni rahisi kuku-shukuru 
Wakati yanapotokea mema 
Ila ni ngumu kuamini 
Kuwa hata na magumu nayo Mungu umeyaruhusu 
Kwa kuniwazia mema 

Umeruhusu mazuri nifurahi, tena nikushukuru 
Na mabaya ili niwe hodari, na kisha nikusifu 
Mbele umeniwekea fahari, haya ni ya muda tu 
Macho yangu yatazama mbali, uliko utukufu

Yote mema yote mema, Yote mema 
Hata magumu yana sababu,
Yote mema, Yote mema 
Sitalaumu sitakufuru 

Sasa nimejua kuwa, wewe uliyenipa samaki 
Ndiwe pia umetaka, wakati mwingine nipate nyoka 
Tena nimejua kuwa, wewe uliyenipa mkate 
Ndiwe pia umetaka, wakati mwingine nipate jiwe 

Umeruhusu mazuri nifurahi, tena nikushukuru 
Na mabaya ili niwe hodari, na kisha nikusifu 
Mbele umeniwekea fahari, haya ni ya muda tu 
Macho yangu yatazama mbali, uliko utukufu 

Yote mema yote mema, Yote mema 
Hata magumu yana sababu,
Yote mema, Yote mema 
Sitalaumu sitakufuru 

Nimejifunza kuwa na shibe tena 
Nimejifunza kuwa na njaa tena 
Kuwa nacho hata kuwa nacho 
Najua yote yanafanya kazi, ili kunipatia mema 
Yamefanyika kama kazi, ukamalifu wake

Yote mema yote mema, Yote mema 
Hata magumu yana sababu,
Yote mema, Yote mema 
Sitalaumu sitakufuru 

Yote mema yote mema, Yote mema 
Hata magumu yana sababu,
Yote mema, Yote mema 
Sitalaumu sitakufuru 

Yote Mema VideoShare:

Write a review/comment/correct the lyrics of Yote Mema:

0 Comments/Reviews