Chorus / Description :
Wakati wote niwe nawe (Baba)
Machozi yangu yafute (Mungu)
Asante kwa yote (Baba)
Nimekuwa jasiri (Asante)
Asante kwa yote mema
(asante kwa yote)
Ni rahisi moyo lawama linapotokea mbaya
Ninasahau hayo yote ni mpango wako
Ninapata shida kichwani ninachanganyikiwa
Nikumbushe wema wako, wakati wote nikuabudu
Nikusifu kwa hali zote nisiende mbali nawe
Wakati wote niwe nawe (Baba)
Machozi yangu yafute (Mungu)
Wakati wote niwe nawe (Bwana)
Machozi yangu yafute (Mungu)
Ni wewe ndiwe mfariji wapekee
Baba wa yatima, mume wa wajane
Niwezeshe kustahimili kiangazi na masika
Pepo mbaya na mzuri pale unaponipitia
Nisimame mbele zako milele milele
Nishike na mkono wako daima daima
Maana kila litokalo wewe umepanga litokee
Sio kwamba nia yako tupotee ila tuzidishe imani
Wakati wote niwe nawe (Baba)
Machozi yangu yafute (Mungu)
Wakati wote niwe nawe (Bwana)
Machozi yangu yafute (Baba)
Asante kwa yote (Baba)
Nimekuwa jasiri (Asante)
Asante kwa yote mema
(asante kwa yote)
Kwa utukufu wako (asante)
Asante Baba (asante)
Pokea moyo shukurani (asante kwa yote)
Oh Baba (asante )
Nakushukuru kwa njia zako (asante)
Nakushukuru kwa matendo yako (asante)