Alice Kamande Nimfahamu Yesu - Nataka nimjue Yesu zaidi Lyrics

Nataka nimjue Yesu
Na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili

Nataka nimwone Yesu
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni
Kujidhihirisha kwangu

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili

Nataka nimfahamu
Na nizidi kupambanua
Mapenzi yake nione
Yale yanayo pendeza

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili

Nataka nikae nawe
Kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonesha
Wengine wokovu wake

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili

Nimfahamu Yesu - Nataka nimjue Yesu zaidi Video



Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Nimfahamu Yesu - Nataka Nimjue Yesu Zaidi :

0 Comments/Reviews