1 Yohana Mlango 1 1st John

1 Yohana 1:1 1stJohn 1:1

Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;

1 Yohana 1:2 1stJohn 1:2

(na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

1 Yohana 1:3 1stJohn 1:3

hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.

1 Yohana 1:4 1stJohn 1:4

Na haya twayaandika, ili furaha yetu itimizwe.

1 Yohana 1:5 1stJohn 1:5

Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.

1 Yohana 1:6 1stJohn 1:6

Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

1 Yohana 1:7 1stJohn 1:7

bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

1 Yohana 1:8 1stJohn 1:8

Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.

1 Yohana 1:9 1stJohn 1:9

Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

1 Yohana 1:10 1stJohn 1:10

Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.