1 Wathesalonike Mlango 1 1st Thessalonians

1 Wathesalonike 1:1 1stThessalonians 1:1

Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.

1 Wathesalonike 1:2 1stThessalonians 1:2

Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.

1 Wathesalonike 1:3 1stThessalonians 1:3

Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.

1 Wathesalonike 1:4 1stThessalonians 1:4

Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu;

1 Wathesalonike 1:5 1stThessalonians 1:5

ya kwamba injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.

1 Wathesalonike 1:6 1stThessalonians 1:6

Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.

1 Wathesalonike 1:7 1stThessalonians 1:7

Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.

1 Wathesalonike 1:8 1stThessalonians 1:8

Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote.

1 Wathesalonike 1:9 1stThessalonians 1:9

Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;

1 Wathesalonike 1:10 1stThessalonians 1:10

na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.