Hosea Mlango 12 Hosea

Hosea 12:1 Hosea 12:1

Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.

Hosea 12:2 Hosea 12:2

Bwana naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.

Hosea 12:3 Hosea 12:3

Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;

Hosea 12:4 Hosea 12:4

Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;

Hosea 12:5 Hosea 12:5

Naam, Bwana, Mungu wa majeshi; Bwana ndilo kumbukumbu lake.

Hosea 12:6 Hosea 12:6

Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.

Hosea 12:7 Hosea 12:7

Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.

Hosea 12:8 Hosea 12:8

Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.

Hosea 12:9 Hosea 12:9

Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.

Hosea 12:10 Hosea 12:10

Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.

Hosea 12:11 Hosea 12:11

Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.

Hosea 12:12 Hosea 12:12

Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu, Na Israeli alitumika apate mke; Ili apate mke alichunga kondoo.

Hosea 12:13 Hosea 12:13

Na kwa nabii Bwana alimtoa Israeli katika Misri, Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.

Hosea 12:14 Hosea 12:14

Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.