Hosea Mlango 6 Hosea

Hosea 6:1 Hosea 6:1

Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.

Hosea 6:2 Hosea 6:2

Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.

Hosea 6:3 Hosea 6:3

Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.

Hosea 6:4 Hosea 6:4

Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.

Hosea 6:5 Hosea 6:5

Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinywa vya manabii; nimewaua kwa maneno ya kinywa changu; na hukumu yangu itatokea kama mwanga.

Hosea 6:6 Hosea 6:6

Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.

Hosea 6:7 Hosea 6:7

Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.

Hosea 6:8 Hosea 6:8

Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu.

Hosea 6:9 Hosea 6:9

Na kama vile makundi ya wanyang'anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.

Hosea 6:10 Hosea 6:10

Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi.

Hosea 6:11 Hosea 6:11

Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu.