Hosea Mlango 4 Hosea

Hosea 4:1 Hosea 4:1

Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.

Hosea 4:2 Hosea 4:2

Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu.

Hosea 4:3 Hosea 4:3

Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na kila mtu akaaye ndani yake atadhoofika, pamoja na wanyama wa kondeni na ndege wa angani; naam, samaki wa baharini pia wataondolewa.

Hosea 4:4 Hosea 4:4

Walakini asishindane mtu, wala mtu asikemee; maana watu wako ni kama wao washindanao na kuhani.

Hosea 4:5 Hosea 4:5

Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako.

Hosea 4:6 Hosea 4:6

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Hosea 4:7 Hosea 4:7

Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi; nami nitageuza utukufu wao kuwa aibu.

Hosea 4:8 Hosea 4:8

Hujilisha dhambi ya watu wangu, hujifurahisha moyo kwa uovu wao.

Hosea 4:9 Hosea 4:9

Hata itakuwa, kama walivyo watu, ndivyo atakavyokuwa kuhani; nami nitawaadhibu kwa ajili ya njia zao, na kuwalipa kwa matendo yao.

Hosea 4:10 Hosea 4:10

Nao watakula, lakini hawatashiba; watafanya zinaa, lakini hawataongezeka; kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana.

Hosea 4:11 Hosea 4:11

Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.

Hosea 4:12 Hosea 4:12

Watu wangu hutaka shauri kwa gongo lao, na fimbo yao huwahubiri mambo; maana roho ya uzinzi imewakosesha, nao wamekwenda kuzini mbali na Mungu wao.

Hosea 4:13 Hosea 4:13

Hutoa dhabihu juu ya vilele vya milima, na kufukiza uvumba juu ya vilima, chini ya mialoni na milibua na miela, kwa kuwa uvuli wake ni mwema; kwa sababu hiyo binti zenu huzini, na bibi arusi zenu hufanya uasherati.

Hosea 4:14 Hosea 4:14

Sitawaadhibu binti zenu wazinipo, wala bibi arusi zenu wafanyapo uasherati; maana wao wenyewe huenda kando pamoja na wanawake wazinzi, hutoa dhabihu pamoja na makahaba; na watu hawa wasiofahamu wataangamia.

Hosea 4:15 Hosea 4:15

Ingawa wewe, Israeli, unafanya uzinzi, lakini asiasi Yuda; nanyi msiende Gilgali wala msipande mpaka Beth-Aveni, wala msiape mkisema, Aishivyo Bwana.

Hosea 4:16 Hosea 4:16

Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! Bwana atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye nafasi!

Hosea 4:17 Hosea 4:17

Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache.

Hosea 4:18 Hosea 4:18

Kileo chao kimegeuka kuwa uchungu; huzini daima; wakuu wake hupenda aibu.

Hosea 4:19 Hosea 4:19

Upepo umemfunikiza kwa mbawa zake; nao watatahayarika kwa sababu ya dhabihu zao.