Hosea Mlango 1 Hosea

Hosea 1:1 Hosea 1:1

Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Hosea, mwana wa Beeri, siku za Uzia, na Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli.

Hosea 1:2 Hosea 1:2

Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Hosea 1:3 Hosea 1:3

Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Diblaimu; naye akachukua mimba, akamzalia mtoto mwanamume.

Hosea 1:4 Hosea 1:4

Bwana akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.

Hosea 1:5 Hosea 1:5

Tena itakuwa siku ile, nitauvunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli.

Hosea 1:6 Hosea 1:6

Akachukua mimba tena, akazaa mtoto mwanamke. Bwana akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena,nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.

Hosea 1:7 Hosea 1:7

Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa Bwana, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.

Hosea 1:8 Hosea 1:8

Basi, akiisha kumwachisha Lo-ruhama, akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamume.

Hosea 1:9 Hosea 1:9

Bwana akasema, Mwite jina lake Lo-ami kwa maana ninyi si watu wangu,wala mimi sitakuwa MUNGU wenu.

Hosea 1:10 Hosea 1:10

Tena itakuwa ya kwamba hesabu ya wana wa Israeli itafanana na mchanga wa bahari, usioweza kupimwa wala kuhesabiwa; tena itakuwa, badala ya kuambiwa, Ninyi si watu wangu, wataambiwa, Ninyi ndio wana wa Mungu aliye hai.

Hosea 1:11 Hosea 1:11

Na wana wa Yuda na wana wa Israeli watakusanyika pamoja, nao watajiwekea kichwa kimoja, nao watakwea watoke katika nchi hii; kwa maana siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.