Hosea Mlango 8 Hosea

Hosea 8:1 Hosea 8:1

Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, anakuja juu ya nyumba ya Bwana; kwa sababu wamelihalifu agano langu, wameiasi sheria yangu.

Hosea 8:2 Hosea 8:2

Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua.

Hosea 8:3 Hosea 8:3

Israeli ameyatupa yaliyo mema; adui watamfuatia.

Hosea 8:4 Hosea 8:4

Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nalikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.

Hosea 8:5 Hosea 8:5

Amemtupa ndama yako, Ee Samaria; hasira yangu imewaka juu yao; siku ngapi zitapita kabla ya hao kupata hali isiyo na hatia?

Hosea 8:6 Hosea 8:6

Maana katika Israeli kimetokea hata na kitu hiki; fundi ndiye aliyekifanya, nacho si mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande.

Hosea 8:7 Hosea 8:7

Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.

Hosea 8:8 Hosea 8:8

Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.

Hosea 8:9 Hosea 8:9

Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa mwituni aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.

Hosea 8:10 Hosea 8:10

Naam, ijapokuwa waajiri kati ya mataifa, sasa nitawakusanya; nao wanaanza kupunguka kwa sababu ya mzigo wa mfalme wa wakuu.

Hosea 8:11 Hosea 8:11

Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake.

Hosea 8:12 Hosea 8:12

Nijapomwandikia sheria yangu katika amri elfu kumi, zimehesabiwa kuwa ni kitu kigeni.

Hosea 8:13 Hosea 8:13

Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini Bwana hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.

Hosea 8:14 Hosea 8:14

Maana Israeli amemsahau Muumba wake, naye amejenga nyumba za enzi; na Yuda ameongeza miji yenye maboma; lakini nitapeleka moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.