Zekaria Mlango 11 Zechariah

Zekaria 11:1 Zechariah 11:1

Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako.

Zekaria 11:2 Zechariah 11:2

Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.

Zekaria 11:3 Zechariah 11:3

Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi! Kwa maana utukufu wao umeharibika; Sauti ya ngurumo ya wana-simba! Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.

Zekaria 11:4 Zechariah 11:4

Bwana, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,

Zekaria 11:5 Zechariah 11:5

ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe Bwana, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

Zekaria 11:6 Zechariah 11:6

Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema Bwana; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.

Zekaria 11:7 Zechariah 11:7

Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa.

Zekaria 11:8 Zechariah 11:8

Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.

Zekaria 11:9 Zechariah 11:9

Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe.

Zekaria 11:10 Zechariah 11:10

Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.

Zekaria 11:11 Zechariah 11:11

Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la Bwana.

Zekaria 11:12 Zechariah 11:12

Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu.

Zekaria 11:13 Zechariah 11:13

Kisha Bwana akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya Bwana.

Zekaria 11:14 Zechariah 11:14

Ndipo nikaikata vipande viwili fimbo yangu ya pili, iitwayo Vifungo, ili nipate kuuvunja udugu uliokuwa kati ya Yuda na Israeli.

Zekaria 11:15 Zechariah 11:15

Bwana akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu.

Zekaria 11:16 Zechariah 11:16

Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.

Zekaria 11:17 Zechariah 11:17

Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.