Zekaria Mlango 6 Zechariah

Zekaria 6:1 Zechariah 6:1

Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba.

Zekaria 6:2 Zechariah 6:2

Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi;

Zekaria 6:3 Zechariah 6:3

na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.

Zekaria 6:4 Zechariah 6:4

Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu?

Zekaria 6:5 Zechariah 6:5

Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote.

Zekaria 6:6 Zechariah 6:6

Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wakatoka wakafuata nyuma yao; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hata nchi ya kusini.

Zekaria 6:7 Zechariah 6:7

Na wale wekundu wakatoka, wakataka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia.

Zekaria 6:8 Zechariah 6:8

Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.

Zekaria 6:9 Zechariah 6:9

Neno la Bwana likanijia, kusema,

Zekaria 6:10 Zechariah 6:10

Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo enenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli;

Zekaria 6:11 Zechariah 6:11

naam, pokea fedha na dhahabu, ukafanye taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;

Zekaria 6:12 Zechariah 6:12

ukamwambie, ukisema, Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la Bwana.

Zekaria 6:13 Zechariah 6:13

Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.

Zekaria 6:14 Zechariah 6:14

Na hizo taji zitakuwa za Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; ziwe ukumbusho katika hekalu la Bwana.

Zekaria 6:15 Zechariah 6:15

Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la Bwana, nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya Bwana, Mungu wenu.