Zekaria Mlango 5 Zechariah

Zekaria 5:1 Zechariah 5:1

Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo.

Zekaria 5:2 Zechariah 5:2

Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi.

Zekaria 5:3 Zechariah 5:3

Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili.

Zekaria 5:4 Zechariah 5:4

Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.

Zekaria 5:5 Zechariah 5:5

Ndipo yule malaika aliyesema nami akatokea, akaniambia, Inua macho yako sasa, uone ni kitu gani kitokeacho.

Zekaria 5:6 Zechariah 5:6

Nikasema, Ni kitu gani? Akasema, Kitu hiki ni efa itokeayo. Tena akasema, Huu ndio uovu wao katika nchi hii yote;

Zekaria 5:7 Zechariah 5:7

na tazama, talanta ya risasi iliinuliwa; na tazama, mwanamke akaaye katikati ya hiyo efa.

Zekaria 5:8 Zechariah 5:8

Akasema, Huyu ni Uovu; akamtupa chini katikati ya ile efa; akalitupa lile jiwe la risasi juu ya mdomo wa ile efa.

Zekaria 5:9 Zechariah 5:9

Ndipo nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, wanawake wawili walitokea, nao upepo ulikuwa katika mabawa yao; na mabawa yao yalikuwa kama mabawa ya korongo; wakaiinua ile efa kati ya dunia na mbingu.

Zekaria 5:10 Zechariah 5:10

Ndipo nikamwambia yule malaika aliyesema nami, Hawa wanaipeleka wapi efa hii?

Zekaria 5:11 Zechariah 5:11

Akaniambia, Wanakwenda kumjengea nyumba katika nchi ya Shinari; tena ikiisha kutengenezwa, atawekwa huko mahali pake mwenyewe.