Bony Mwaitege - Utanitambuaje - Tazama Matendo

Chorus / Description : Utanitambuaje kama nimeokoka?
Utanitambuaje kama namweshimu Mungu?
Nasema, utajuaje kama tuko pamoja
Katika safari ndefu ya kwenda mbiguni eeh?
Utanitambuaje ndugu yangu nakuuliza niambie aiyee
Matendo tazama matendo
Matendo tazama matendo
Matendo, Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Utanitambuaje - Tazama Matendo Lyrics

Utanitambuaje kama nimeokoka?
Utanitambuaje kama namweshimu Mungu?
Nasema, utajuaje kama tuko pamoja
Katika safari ndefu ya kwenda mbiguni eeh?
Utanitambuaje ndugu yangu nakuuliza niambie aiyee

Huwezi kunitambua kama nimeokoka, kwa kunitazama sura yangu
Huwezi kunitambua kama nimeokoka kwa kunitazama maumbile yangu
Bwana asifiwe isiwe sababu kukufanya uamini kuwa nimeokoka
Japo mali yangu naweza kutamka Bwana asifiwe kumbe sijaokoka
Utanitambuaje niambie aiyee

Ukitaka kutambua kama nimeokoka
Hakuna haja ya kupata shida
Ukitaka kutambua kama nimeokoka
Hakuna haja ya kuumiza kichwa
Bwana wetu Yesu alishasema
Utawatambua kwa matendo
Matendo tazama matendo utanitambua eeh

Matendo yangu, tazama matendo
Matendo tazama matendo
Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Usinitazame umbile tazama matendo
Matendo tazama matendo
Matendo tazama matendo
Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje
Hata kama nimebatizwa tazama matendo
Matendo tazama matendo
Matendo Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Mtume Petro aliulizwa wewe ni mwanafunzi wa Yesu.
Mtume Petro kwa kuogopa wayahudi akakataa mimi simjui Yesu
Wakamwambia mbona hata kusema kwako
Kunaonyesha wewe mwanafunzi wa Yesu
Mtume Petro akaamua kuondoka
Hata hivyo wakamtambua mwendo wake
Wakamwambia mbona hata kutembea kwako
Kunaonyesha wewe mwanafunzi wa Yesu
Kuongea na kutembea kwake Petro
Kulionyesha yeye mwanafunzi wa Yesu
Matendo yangu matendo tazameni matendo utanitambua eeh

Matendo tazama matendo
Matendo tazama matendo
Matendo, Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Ukitaka kutambua kama nimeokoka
Usitazame jinsi ninavojisifia
Naweza kujisifu mimi ni mpole sana
Lakini matendo yangu yakakataa
Naweza kujisifu mimi nawajali sana yatima
Lakini matendo yangu yakakataa
Naweza kujisifu mimi nawajali sana wajane
Lakini matendo yangu yakakataa
Matendo yangu matendo
Kama kweli ninamcha Mungu utanitambua aiyee

Utanitambuaje - Tazama Matendo Video

  • Song: Utanitambuaje - Tazama Matendo
  • Artist(s): Bony Mwaitege
Utanitambuaje - Tazama Matendo

Share: