Bony Mwaitege - Yesu Yupo

Chorus / Description :
Jamani Yesu Yupo
Ni kweli Yesu Yupo
Ni kweli Yesu Yupo
Tunamtangaza yupo
Tumeona kazi zake

Yesu Yupo Lyrics

Jamani Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Tunamtangaza yupo 
Tumeona kazi zake x3

Nilikuwa ninasimuliwa miujiza ya Yesu 
Nimeona kwa macho yangu nimejua yupo
Nilikuwa ninasimuliwa kwamba Yesu anaponya 
Nimeona kwa macho yangu nimejua Yupo 
Ona wengi majambazi Yesu kawabadilisha 
Nimeona kwa macho yangu nimejua yupo 
Waliokuwa machangundoa sasa hivi ni wahubiri 
Yesu kawabadilisha nimejua yupo 
Jamani Yesu yupo, ndugu zangu Yesu yupo 
Ninatangaza yupo, nimeona kazi zake 

Jamani Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Tunamtangaza yupo 
Tumeona kazi zake x3

Lazaro alikuwa kaburini zimepita siku nne 
Yesu alimwita Lazaro akafufuka x2 
Watu walishangaa kumuona Lazaro 
Akifunguliwa sanda na kuanza kutembea X2 
Jamani Yesu yupo, ndugu zangu Yesu yupo 
Tunatangaza yupo, tumeona kazi zake 

Jamani Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Tunamtangaza yupo 
Tumeona kazi zake x3

Likitajwa jina lake 
Mashetani yanapiga kelele 
Yanwatoka watu ni kweli Yesu yupo 
Likitajwa jina lake 
Majini yanapiga kelele 
Yanwatoka watu ni kweli Yesu yupo 
Wagonjwa wamefunguliwa 
Kwa macho tunaona 
Yesu afanye nini ili tujue yupo 

Jamani Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Ni kweli Yesu Yupo 
Tunamtangaza yupo 
Tumeona kazi zake x3

Yesu Yupo Video

  • Song: Yesu Yupo
  • Artist(s): Bony Mwaitege


Share: