Shukrani Lyrics

By Christ Ambassadors

Lyrics

Bwana wangu naomba unisikie  

Nijapo mbele zako 

(Naomba unisikie, naomba unisikie) 

Wimbo wangu siku ya leo si mwingine 

Bali ni wimbo wa shukrani 

(Bwana asante, kwa yote umenitendea) 


Leo naamua kubadili mtazamo wangu Baba 

Unajua muda mwingi nijapo mbele zako 

Huwa naja nikilalamika 

Lakini leo naleta shukrani shukrani 

oh wastahili shukrani Baba 


Muda wowote nikipatwa na jambo baya 

Siwezi sahau kulalamika 

(Kawaida ya mwanadamu, mwepesi wa kulalamika) 

Lakini kwa mazuri muda mwingi huwa nachukulia kawaida 

(Leo nakuja kwa sauti ya shukrani) 


Leo naamua kubadili mtazamo wangu Baba 

Unajua muda mwingi nijapo mbele zako 

Huwa naja nikilalamika 

Lakini leo naleta shukrani shukrani 

oh wastahili shukrani Baba 


Inapendeza kuja mbele zako 

Na sauti za shukrani ewe bwana wangu. 

(Inatupasa wanadamu kukushukuru daima) 

Ni vyema kuwa na shukrani nyingi 

kuliko malalamiko ooh oh. 

(Leo twakuja kwa sauti ya shukrani) 


Leo naamua kubadili mtazamo wangu Baba 

Unajua muda mwingi nijapo mbele zako 

Huwa naja nikilalamika 

Lakini leo naleta shukrani shukrani 

oh wastahili shukrani Baba 

SHUKRANI, AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR 2019, Copyright Reserved

Now Playing...