Yatupasa Kushukuru

By Christ Ambassadors

Lyrics

Hebu tu tafakari

Mungu atutendeayo

Jinsi anavyo tujali

Jinsi anayo nilinda

Uhai wetu upitao tumsifu ungalipo


Ni ya ajabu sana

Matendo ya bwana Mungu

Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa

Lakini bwana ni mwema kwetu

Hawezi tuacha


Japo mengi hayajakwisha 

Yatubidishayo tumshukuru Mungu wetu 

Japo twapita majaribu mengi 

Bado yapo mengi yakushukuriwa 

Eeh ee jiunge nasi 

Tulisisitize jambo hili la muhimu 

Yale yote tujiulizayo moyoni 

Majibu anayo Mungu wetu


Tuwapo safarini

Kifo kina tuandama

Tafakari safari zote

Kumbuka ile ajali

Ulifanya nini mpendwa ukatoka umzima


Ni ya ajabu sana

Matendo ya bwana Mungu

Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa

Lakini bwana ni mwema kwetu

Hawezi tuacha


Ni ya ajabu sana

Matendo ya bwana Mungu

Twapasa kushukuru kwa baraka anazotupa

Hakuna kitu wacha uhai ni yeye Mungu pekee


Tulalapo usiku

Twalala kama wafuu

Asubuhi kunapo kucha

Twadumu kuwa wazima

Ni ratiba yake tusifu

Ni mipango yake kwetu


Ni ya ajabu sana

Matendo ya bwana Mungu

Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa

Lakini bwana ni mwema kwetu

Hawezi tuacha


Ni ya ajabu sana

Matendo ya bwana Mungu

Twapasa kushukuru

Kwa baraka anazotupa

Hakuna kitu wacha uhai ni ye Mungu pekee


Ohh bwana ni mwema kwetu

Hawezi tuacha 3

YATUPASA KUSHUKURU, AMBASSADORS OF CHRIST CHOIR, COPYRIGHT RESERVED 2013