Chorus / Description :
Wacha nisanitize
Oh barakoa kigodo nisishike pua
Mmh Wacha nisanitize
Barakoa kigodo nisishike pua
Haloo papa ni mimi mwanao
Hii namb nimechukua Yeremiah hapa
Inasema niite nitakuitikia
Nitakuonyesha magumu usiyoyajua mwanangu .
Haya leo simu yangu hii napiga kwa imani
Nakuomba sikiliza daddy
Naumia moyoni, unaweza tunusuru na hili
Manabii wale baba ungewaambia kuna corona
Au tunadanganywa ni bandia wanayoona
Je umekaa kimya ukitazama wanayofanya .
Mbona mwaka jana walituambia huu ni
Mwaka wa Bwana
Tumekaa mwaka ulianza shwari
Sasa hivi hatuelewi
Kila saa alama ya hatari ni mbaya habari
Wamekufa saba walikufa sita
Mara ooh mnadanganywa wamefika kumi .
Wacha nisanitize
Oh barakoa kigodo nisishike pua
Mmh Wacha nisanitize
Barakoa kigodo nisishike pua .
Wakati nasubiri
Heri matajiri tajiri
Wanaweza kununua maski
Wengine sis hizo bei zake
Ndio tunategemea tule
Mama mama muda wote ni pressure
Maana watoto wake maisha ndo wanatafuta
Kwa siku kupata kwa siku tumezoea .
Usipotuhurumia wewe ndio tumekwisha
Usipotuhurumia wewe ndio tumekwisha
Niliongea na waombaji
Nikawaambia tusiache kuomba
Maana adui ametumia mabaya
Mi nakuamini kuamini kuamini Baba .
Wacha nisanitize
Oh barakoa kigodo nisishike pua
Mmh Wacha nisanitize
Barakoa kigodo nisishike pua