Chorus / Description :
Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana
Usisahau fadhili zake zote
Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana
Usisahau fadhili zake zote
Lihimidi Jina lake Jina lake Jina lake Takatifu
Lihimidi jina lake, Jina lake, jina lake Takatifu
Mashariki na magharibi haziwezi kutana
Hivyo ndivyo uliweka dhambi zangu mbali nami
Kwa kukomboa uhai wangu wanisamehe
Tena wanivisha taji ya upendo wako
Ooh Nisemeje? Nikupe nini?
Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana
Usisahau fadhili zake zote
Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana
Usisahau fadhili zake zote
Lihimidi Jina lake Jina lake Jina lake Takatifu
Lihimidi jina lake, Jina lake, jina lake Takatifu
Kweli Baba wewe ni mwema, uinuliwe
Kwa ajili ya neema na fadhili zako
Jina lako litukuzwe leo na milele
Maana haulinganiswi na yeyote Baba
Nisemeje nikupe nini ila sifa
Upendo wako umenizunguka
Neema yako imenipandisha
Halleluya, jina lako ni kuu
Amani na furaha umenipa
Halleluya, jina lako ni kuu
Astahili sifa, astahili utukufu
Takatifu uu Baba