Chorus / Description :
Katika maisha yangu nilipokea wageni,
Nikawakaribisha kwangu, wakafanya vitu vingi
Katika maisha yangu nilipokea wageni,
Nikawakaribisha kwangu, wakafanya vitu vingi
Hawakuwa wa kudumu, walikuwa wapitaji
Ila moyo wa ukarimu, ukanisababishia machozi
Mgeni wa kwanza alikuwa ni uchungu,
Akaniumiza, akanipa maumivu
Alipomaliza akaenda zake,
Mgeni wa pili alikuwa ni huzuni,
Huyu naye
Akanikosesha furaha,
Mgeni wa tatu alikuwa ni magonjwa,
Akanidhoofisha, akataka kuniua
Hakufanikiwa akaenda zake
Aliyefuata alininyima watoto
Jina lake tasa, naye alipita
Mgeni mmoja jina lake ni mauti
Akamchukua Ntimi, akaniachia jeraha
Mgeni mwingine jina lake hofu
Hakutaka nifanikiwe, akanipa fikra potofu
Nikajiona siwezi, tena nitafeli
Huyo naye alipita
Hawa ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Hawa ni wageni, tena wapitaji
Hawatadumu, watapita
Hakuna jambo lolote gumu
Litakalodumu kwenye maisha yako
Ila yote yatapita
Na yakishapita,
Hayatarudi tena
Tough times never last,
But tough people do
Mapito siyo mambo magumu unayoyapitia kwenye maisha yako,
Ila mapito ni mambo magumu yanayopita kwenye maisha yako,
Ndiyo maana ninaita mapito, kwa kuwa yanapita tu, na yanapita kwenye maisha yako,
Na yakishapita hayawezi kurudi tena, Hah
Magonjwa,
Hao ni wageni, tena wapitaji, Hawatadumu, watapita
Uchungu, (Huzuni)
Hao ni wageni, tena wapitaji, Hawatadumu, watapita
Mateso, (Changamoto)
Hao ni wageni, tena wapitaji, Hawatadumu, watapita
(Hata dhiki)
Hao ni wageni, tena wapitaji, Hawatadumu, watapita