1 Timotheo Mlango 3 1st Timothy

1 Timotheo 3:1 1stTimothy 3:1

Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.

1 Timotheo 3:2 1stTimothy 3:2

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;

1 Timotheo 3:3 1stTimothy 3:3

si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;

1 Timotheo 3:4 1stTimothy 3:4

mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;

1 Timotheo 3:5 1stTimothy 3:5

(yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)

1 Timotheo 3:6 1stTimothy 3:6

Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.

1 Timotheo 3:7 1stTimothy 3:7

Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.

1 Timotheo 3:8 1stTimothy 3:8

Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.

1 Timotheo 3:9 1stTimothy 3:9

wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.

1 Timotheo 3:10 1stTimothy 3:10

Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.

1 Timotheo 3:11 1stTimothy 3:11

Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.

1 Timotheo 3:12 1stTimothy 3:12

Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.

1 Timotheo 3:13 1stTimothy 3:13

Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

1 Timotheo 3:14 1stTimothy 3:14

Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu.

1 Timotheo 3:15 1stTimothy 3:15

Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.

1 Timotheo 3:16 1stTimothy 3:16

Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.