1 Timotheo Mlango 4 1st Timothy

1 Timotheo 4:1 1stTimothy 4:1

Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

1 Timotheo 4:2 1stTimothy 4:2

kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

1 Timotheo 4:3 1stTimothy 4:3

wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

1 Timotheo 4:4 1stTimothy 4:4

Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

1 Timotheo 4:5 1stTimothy 4:5

kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

1 Timotheo 4:6 1stTimothy 4:6

Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.

1 Timotheo 4:7 1stTimothy 4:7

Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.

1 Timotheo 4:8 1stTimothy 4:8

Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.

1 Timotheo 4:9 1stTimothy 4:9

Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;

1 Timotheo 4:10 1stTimothy 4:10

kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.

1 Timotheo 4:11 1stTimothy 4:11

Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.

1 Timotheo 4:12 1stTimothy 4:12

Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

1 Timotheo 4:13 1stTimothy 4:13

Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha.

1 Timotheo 4:14 1stTimothy 4:14

Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.

1 Timotheo 4:15 1stTimothy 4:15

Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.

1 Timotheo 4:16 1stTimothy 4:16

Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.