1 Timotheo Mlango 2 1st Timothy

1 Timotheo 2:1 1stTimothy 2:1

Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

1 Timotheo 2:2 1stTimothy 2:2

kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.

1 Timotheo 2:3 1stTimothy 2:3

Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;

1 Timotheo 2:4 1stTimothy 2:4

ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.

1 Timotheo 2:5 1stTimothy 2:5

Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;

1 Timotheo 2:6 1stTimothy 2:6

ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.

1 Timotheo 2:7 1stTimothy 2:7

Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.

1 Timotheo 2:8 1stTimothy 2:8

Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.

1 Timotheo 2:9 1stTimothy 2:9

Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

1 Timotheo 2:10 1stTimothy 2:10

bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.

1 Timotheo 2:11 1stTimothy 2:11

Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.

1 Timotheo 2:12 1stTimothy 2:12

Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

1 Timotheo 2:13 1stTimothy 2:13

Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.

1 Timotheo 2:14 1stTimothy 2:14

Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.

1 Timotheo 2:15 1stTimothy 2:15

Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.