Chorus / Description :
Tunatimiza maandiko, Tumekuja kukuchukua
Kama ilivyoandikwa, Tumekuja kukuchukua wewe
Mtu ataacha wazazi wake, Tumekuja kukuchukua
Ataambatana na mumewe, Tumekuja kukuchukua
Bibi arusi twende wee, Tumekuja kukuchukua
Malkia wetu twende, Tumekuja kukuchukua
Usiogope twende, Tumekuja kukuchukua
Yanatimizwa maandiko, Tumekuja kukuchukua
ieyee yaah hayaa yeeh
Tumekuja kukuchukua
ieyee yaah hayaa yeeh
Tumekuja kukuchukua
Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua)
Bibi harusi twende mama (Tumekuja kukuchukua)
Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua)
Wazazi wako tumeelewana nao (Tumekuja kukuchukua)
Wameturuhusu tuondoke nawe (Tumekuja kukuchukua)
Tusingeweza kukuchukua bila ruhusa ya wazazi wako
Ndio maana tulisafiri kwenda kuwaomba wazazi wako
Ili turuhusiwe, zawadi mbali mbali tuliwapelekea
Tunashukuru Mungu walizipokea
Tulipowaomba tukuchukue
Kuna taratibu tuliambiwa tuzifuate
Taratibu zote tulizifwata,
Hapo ndipo tuliporuhusiwa
Tumepewa baraka zote wewe uwe mke wa kijana wetu
Bibi arusi wewe
Tumepewa baraka zote wewe uingie kwenye ukoo wetu
Bibi arusi wee
Tunamshukuru Jehovah (Tumekuja kukuchukua)
Maombi yetu ameyasikia (Tumekuja kukuchukua)
Tumeomba muda mrefu sana (Tumekuja kukuchukua)
Kijana wetu apate mke (Tumekuja kukuchukua)
Maombi yetu yamejibiwa (Tumekuja kukuchukua)
Wewe ndiye jibu la maombi yetu (Tumekuja kukuchukua)
Sisi unaotuona (Tumekuja kukuchukua)
Ni ndugu wa Bwana arusi (Tumekuja kukuchukua)
Tumesindikiza ndugu yetu (Tumekuja kukuchukua)
Tumekuja kukuchukua wewe (Tumekuja kukuchukua)
Tunawashukuru ndugu zako (Tumekuja kukuchukua)
Wametupokea vizuri sana (Tumekuja kukuchukua)
Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua)
Twende kwetu mama
Tunatimiza maandiko (Tumekuja kukuchukua)
Kama ilivyoandikwa (Tumekuja kukuchukua wewe)
Mtu ataacha wazazi wake (Tumekuja kukuchukua)
Ataambatana na mumewe (Tumekuja kukuchukua)
Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua)
Malkia wetu twende (Tumekuja kukuchukua)
Usiogope twende (Tumekuja kukuchukua)
Yanatimizwa maandiko (Tumekuja kukuchukua)