Christopher Mwahangila - Mungu ni Mungu tu

Chorus / Description : Ooh Mungu,(Haleluya Mungu wetu) Mungu ni Mungu tu,atabaki kuwa Mungu tu (Haleluya Mungu wetu)
Ooh Mungu baba, Huyu Mungu wa mbinguni jamani
Huyu Mungu wa elijah, Maishani mwako mama yangu wewe
Mahali pote unapotembea, Ata wainuke wamseme vibaya, Ata wamkatae mbele yako. #IAmWhoIAm

Mungu ni Mungu tu Lyrics

Nabii Elijah, aliwaita manabii wote,wa Mungu baali
Lengo la elija,ilikuwa ni kumthibitisha Mungu wa kweli ni yupi,
kati ya Mungu wa baali, na Mungu wa mbinguni.
Akawambia watu nikaribieni mimi, akachukua mawe kumi na mbili akaanza kujenga madhabau.
Akaweka kuni juu yake,akaweka sadaka juu yake,
Akachimba mfereji ,akawambia watu mwageni maji mapipa manne,
wakamwaga maji mara ya kwanza ,wakamwaga maji mara ya pili,wakamwaga maji mara ya tatu.
Elijah, akaanza kumuita Mungu,Mungu wa mbinguni wewe Mungu,
Mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo.
Moto ukashuka ,ukaramba ile sadaka, ukaramba zile kuni ,ukaramba na yale mawe,
ukaramba na yale mavuno ,ukaramba na yale maji ,
Watu wakasujudu,wakasema huyu ndiye Mungu,anayepaswa kuabudiwa ,
Ndiye Mungu ninaye mwimbia Mungu wa Elijah.

Ooh Mungu,(Haleluya Mungu wetu) Mungu ni Mungu tu,atabaki kuwa Mungu tu (Haleluya Mungu wetu)
Ooh Mungu baba, Huyu Mungu wa mbinguni jamani
Huyu Mungu wa elijah, Maishani mwako mama yangu wewe
Mahali pote unapotembea, Ata wainuke wamseme vibaya, Ata wamkatae mbele yako.

Na wewe ndugu yangu,unayenisikia, unaye nitazama, Unaona nini mbele yako?
pengine unaona majaribuaujui utafanya nini, we mkaribie Mungu tu,
Pengine unaona magonjwa, haujui utapona lini we mkaribie Mungu tu.
Pengine unaona vita kubwa,haujui utashinda vipi, we mkaribie Mungu tu.
Pengine unaona watesi ,haujui utapita vipi, we mkaribie Mungu tu.
Pengine ni jaribu katika ndoa yako,haujui utashinda vipi,we mkaribie Mungu tu.
Hakuna linaloshidikana kwake Mungu, Aliyemshindia elijah ,
Katikati manabii wa baali atakushindia na wewe.

Ooh Mungu,(Haleluya Mungu wetu) Mungu ni Mungu tu,atabaki kuwa Mungu tu
Ooh Mungu baba, Huyu Mungu wa mbinguni jamani
Huyu Mungu wa elijah, Maishani mwako mama yangu wewe
Mahali pote unapotembeaAta wainuke wamseme vibaya, Ata wamkatae mbele yako.

Wanadamu wamekusemea maneno,kwamba hautaweza ,katika jaribu lako,
wanadamu wamekusemea maneno,kwamba hautashinda katika vita yako,
kumbe njia za Mungu, sio sawa na za mwanadamu
mipango ya Mungu ,sio sawa na ya mwanadamu,
akili ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,
Maneno ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,
Mawazo ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,
Kazi ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,
Sauti ya Mungu ,sio sawa na ya mwanadamu
Aliye mshindia elijah ,
katikati ya manabii wa baali atakushindia na wewe.

Ooh Mungu,(Amen Haleluya) Mungu ni Mungu tu,atabaki kuwa Mungu tu
Ooh Mungu baba, Huyu Mungu wa mbinguni jamani
Huyu Mungu wa elijah, Maishani mwako mama yangu wewe
Mahali pote unapotembeaAta wainuke wamseme vibaya, Ata wamkatae mbele yako.

Mungu ni Mungu tu Video

  • Song: Mungu ni Mungu tu
  • Artist(s): Christopher Mwahangila


Share: