Maumivu ya Jaribu

by Martha Mwaipaja

Japo jaribu limeruhusiwa na wewe Mungu

Hili jaribu linaumiza moyo 

Japo jaribu limeruhusiwa na wewe mwenyewe 

Hili jaribu linaumiza moyo 

Japo maumivu haya Yesu anajua 

Moyo wangu unateseka aah


Japo haya yote wewe pekee wajua 

Lakini moyo wangu unateseka aa

Nitie nguvu baba yangu 


Naishi katikati ya watu 

Wasio jua ni nini napitia 

Natembea katikati ya watu 

Wasio maumivu yangu 

Kwa sababu ya mateso niliyo nayo 

Nimejaribu kuelezea wengi 

Pamoja na kuwaeleza ndio hawa 

hawajaelewa ninavyoteseka 

Nilijua kwa kuwaaleza kwangu 

Watajua nitesekavyo hawakujua 

Japo maumivu haya wewe Yesu wayajua 

Moyo wangu unateseka aah


Hivi naomba kwa unyenyekevu 

Usiniache jaribu likaniweza 

Baba yangu mimi nimekubali kupita 

Lakini usiniache eeh 

Nimekubali kupitia usiniache 

Nikamezwa na jaribu 


Japo Ibrahimu aliitwa Baba wa imani 

Moyo wake uliteseka 

Japo Ibrahimu ulisema naye 

Ukasema utampa watoto bado alilia 

Pamoja na kwamba ulisema naye kwenye 

Mti alipochelewa Isaka Ibrahimu kali 

Japo alijua ni wewe Baba utampatia 

Ibrahimu moyo uliuma 

Kwa sababu Ibrahimu alichelewa kupata mtoto 

Moyo wake uliteseka 

Japo alijua Isaka ni mtoto wa pekee 

Kwa sababu alichelewa alilia 

Alijua utampa watoto wazuri 

Lakini moyo wake ulilia 


Pamoja na kwamba unatufundisha majaribu lazima 

Lakini mioyo inauma 

Usituache Yesu, usituache wanao 

Usituache wanao tukapotea 

Usituache Yesu, usituache Baba 

Usituache wanao tukapotea 

Usituache Yesu, usituache wanao 

Usituache wanao tukapotea 

...


Share