Zabron Singers - Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana

Chorus / Description : Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako

Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana Lyrics

Tumeuona mkono wake Bwana

Mengi mazuri tumeyaona, Mungu umetenda
Ni kweli we muweza
Ulitamka vitu vikawa
Neno tu latosha
Ukisema umetenda
Bahari shamu Isiraeli
Ah uliwavusha
Kawatoa utumwani
Watumishi wako umewapa
Yote waombayo
Ikiwa umependezwa

Uamulo hakuna wa kulipinga
Hakika we ni Mungu, wa vyote
Unatawala dunia na vilivyomo
Makuu umeyatenda, Jehova

Refrain:
Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako

Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako

Ona ona ona ona
Msalabani ulitufia, hm ulitupenda
Dhambi zetu ukabeba
Baraka zako tuliziomba kweli tumeona
Hakika unabariki
Hata vipaji we ndo hutoa umetuwezesha
Tunaimba na kusifu
Walio haki hutowaacha, uliwaahidi
Hata mwisho wa dahari

Hm watu wako umewapa mamlaka
kwa jina lako Yesu
Waponye
Na huna ubaguzi
Wote ni sawa kwako
Umetuita Yesu, tupone

(Refrain)

Ona ona ona
Daima we umwema tutaishi kwako
(Repeat)

Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana Video

  • Song: Mkono Wa Bwana - Tumeuona Mkono Wako Bwana
  • Artist(s): Zabron Singers


Share: