Lyrics Page

Sikuachi Tena

By Zabron Singers

1,733 views Jun 6, 2026 updated

Tunaishi kwa nguvu za Mungu yeye ndo katuweka hapa 

Kila hatua tunapitia ye ndo mlinzi wetu 

Asubuhi ifikapo hujua siku itaenda vipi 

Je ntavuka salama jioni hata usiku 

Kwa dakika sekunde hujua siku itaenda vipi 

Kupata na kukosa anajua mimi nitapata nini 

Kulala kuamka anajua mimi nitaamka vipi 

Maisha yetu yote ndiye anaye siri zetu 


Wewe ni Mungu wangu sikuachi tena 

Mimi kuwepo leo neema zako zaniwezesha 

Sina haki mimi kujisifu tena 

Kwani bila wewe hakika mimi singekuwa hivi 


The light of my way and shining star in my life 

He is the Lord of all lights and victory, and everything is His 

Upatacho shukuru ni Mungu ndiye kakuweka hapo 

Usisahau kumtumikia bado ungali hai 

Kumbuka kuna siku utadaiwa kwa matendo yako 

Iweje jema au baya watu umewatenda vipi 

Je wazitumiaje baraka ulizopewa na Mungu 

Suluhisho pekee ni Mungu pekee tumpe maisha yetu 


Wewe ni Mungu wangu sikuachi tena 

Mimi kuwepo leo neema zako zaniwezesha 

Sina haki mimi kujisifu tena 

Kwani bila wewe hakika mimi singekuwa hivi 


Wewe ni Mungu wangu sikuachi tena 

Mimi kuwepo leo neema zako zaniwezesha 

Sina haki mimi kujisifu tena 

Kwani bila wewe hakika mimi singekuwa hivi 

Official Video

Save Your Favorites

Create a free account to save songs, build your personal library, and connect with the Zion community.

Create Free Account

Join the Zion Community

Create a free account to save your favorite lyrics, submit song suggestions, and connect with fellow worshippers.

No spam. Unsubscribe anytime.