Yoshua Mlango 15 Joshua

Yoshua 15:1 Joshua 15:1

Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.

Yoshua 15:2 Joshua 15:2

Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini;

Yoshua 15:3 Joshua 15:3

nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hata Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafikilia Adari, na kuzunguka kwendea Karka;

Yoshua 15:4 Joshua 15:4

kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini.

Yoshua 15:5 Joshua 15:5

Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;

Yoshua 15:6 Joshua 15:6

na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;

Yoshua 15:7 Joshua 15:7

kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli;

Yoshua 15:8 Joshua 15:8

kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;

Yoshua 15:9 Joshua 15:9

kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hata kufikilia chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hata kufikilia Baala (ndio Kiriath-yearimu);

Yoshua 15:10 Joshua 15:10

kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;

Yoshua 15:11 Joshua 15:11

kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini.

Yoshua 15:12 Joshua 15:12

Na mpaka wa upande wa magharibi ulifikilia hata bahari kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kote kote sawasawa na jamaa zao.

Yoshua 15:13 Joshua 15:13

Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama Bwana alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).

Yoshua 15:14 Joshua 15:14

Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki.

Yoshua 15:15 Joshua 15:15

Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.

Yoshua 15:16 Joshua 15:16

Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe.

Yoshua 15:17 Joshua 15:17

Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.

Yoshua 15:18 Joshua 15:18

Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini?

Yoshua 15:19 Joshua 15:19

Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.

Yoshua 15:20 Joshua 15:20

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.

Yoshua 15:21 Joshua 15:21

Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri;

Yoshua 15:22 Joshua 15:22

na Kina, na Dimona, na Adada;

Yoshua 15:23 Joshua 15:23

na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani;

Yoshua 15:24 Joshua 15:24

na Zifu, na Telemu, na Bealothi;

Yoshua 15:25 Joshua 15:25

na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori);

Yoshua 15:26 Joshua 15:26

na Amamu, na Shema, na Molada;

Yoshua 15:27 Joshua 15:27

na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti;

Yoshua 15:28 Joshua 15:28

na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia;

Yoshua 15:29 Joshua 15:29

na Baala, na Iyimu, na Esemu;

Yoshua 15:30 Joshua 15:30

na Eltoladi, na Kesili, na Horma;

Yoshua 15:31 Joshua 15:31

na Siklagi, na Madmana, na Sansana;

Yoshua 15:32 Joshua 15:32

na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:33 Joshua 15:33

Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna,

Yoshua 15:34 Joshua 15:34

na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu;

Yoshua 15:35 Joshua 15:35

na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka;

Yoshua 15:36 Joshua 15:36

na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:37 Joshua 15:37

Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi;

Yoshua 15:38 Joshua 15:38

na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli;

Yoshua 15:39 Joshua 15:39

na Lakishi, na Boskathi, na Egloni;

Yoshua 15:40 Joshua 15:40

na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi;

Yoshua 15:41 Joshua 15:41

na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:42 Joshua 15:42

Libna, na Etheri, na Ashani;

Yoshua 15:43 Joshua 15:43

na Yifta, na Ashna, na Nesibu;

Yoshua 15:44 Joshua 15:44

na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:45 Joshua 15:45

Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake;

Yoshua 15:46 Joshua 15:46

kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:47 Joshua 15:47

Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake.

Yoshua 15:48 Joshua 15:48

Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko;

Yoshua 15:49 Joshua 15:49

na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri);

Yoshua 15:50 Joshua 15:50

na Anabu, na Eshtemoa, na Animu;

Yoshua 15:51 Joshua 15:51

na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:52 Joshua 15:52

Arabu, na Duma, na Eshani;

Yoshua 15:53 Joshua 15:53

na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka;

Yoshua 15:54 Joshua 15:54

na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:55 Joshua 15:55

Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta;

Yoshua 15:56 Joshua 15:56

na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa;

Yoshua 15:57 Joshua 15:57

na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:58 Joshua 15:58

Halhuli, na Bethsuri, na Gedori;

Yoshua 15:59 Joshua 15:59

na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:60 Joshua 15:60

Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.

Yoshua 15:61 Joshua 15:61

Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka;

Yoshua 15:62 Joshua 15:62

na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 15:63 Joshua 15:63

Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.