Yoshua Mlango 21 Joshua

Yoshua 21:1 Joshua 21:1

Wakati huo hao vichwa vya nyumba za mababa ya Walawi wakamwendea Eleazari, kuhani, na Yoshua, mwana wa Nuni, na hao waliokuwa vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli;

Yoshua 21:2 Joshua 21:2

wakanena nao hapo Shilo katika nchi ya Kanaani, wakisema, Yeye Bwana aliamuru kwa mkono wa Musa kwamba sisi tupewe miji tupate kukaa humo, pamoja na malisho yake kwa ajili ya wanyama wetu wa mifugo.

Yoshua 21:3 Joshua 21:3

Basi wana wa Israeli wakawapa Walawi miji hii, pamoja na malisho yake, katika urithi wao, sawasawa na hiyo amri ya Bwana.

Yoshua 21:4 Joshua 21:4

Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila ya Yuda, na katika kabila ya Simeoni, na katika kabila ya Benyamini.

Yoshua 21:5 Joshua 21:5

Kisha Wakohathi wengine waliosalia walipata kwa kura katika jamaa za kabila ya Efraimu, na katika kabila ya Dani, na katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, miji kumi.

Yoshua 21:6 Joshua 21:6

Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura katika jamaa za kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila ya Manase huko Bashani, miji kumi na mitatu.

Yoshua 21:7 Joshua 21:7

Na wana wa Merari kwa kuandama jamaa zao walipata katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni, miji kumi na miwili.

Yoshua 21:8 Joshua 21:8

Kisha wana wa Israeli waliwapa Walawi kwa kura miji hiyo pamoja na malisho yake, kama Bwana alivyoamuru kwa mkono wa Musa.

Yoshua 21:9 Joshua 21:9

Kisha wakawapa katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina;

Yoshua 21:10 Joshua 21:10

nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao.

Yoshua 21:11 Joshua 21:11

Nao wakawapa Kiriath-arba, huyo Arba alikuwa baba yake Anaki, (ndio Hebroni), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na malisho yake yaliyouzunguka pande zote.

Yoshua 21:12 Joshua 21:12

Lakini mashamba ya mji, na vile vijiji vyake, wakampa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

Yoshua 21:13 Joshua 21:13

Kisha wakawapa wana wa Haruni kuhani Hebroni pamoja na malisho yake, huo mji wa kukimbilia kwa ajili ya mwuaji, na Libna pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:14 Joshua 21:14

na Yatiri pamoja na malisho yake, na Eshtemoa pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:15 Joshua 21:15

na Holoni pamoja na malisho yake, na Debiri pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:16 Joshua 21:16

na Aini pamoja na malisho yake, na Yuta pamoja na malisho yake, na Bethshemeshi pamoja na malisho yake; miji kenda katika kabila hizo mbili.

Yoshua 21:17 Joshua 21:17

Tena katika kabila ya Benyamini, Gibeoni pamoja na malisho yake, na Geba pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:18 Joshua 21:18

na Anathothi pamoja na malisho yake, na Almoni pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:19 Joshua 21:19

Miji yote ya wana wa Haruni, makuhani, ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na malisho yake.

Yoshua 21:20 Joshua 21:20

Na jamaa za wana wa Kohathi, Walawi, hao wana wengine wa Kohathi waliosalia, wao walikuwa na miji ya kura yao katika kabila ya Efraimu.

Yoshua 21:21 Joshua 21:21

Nao wakawapa Shekemu pamoja na malisho yake, katika nchi ya vilima ya Efraimu, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Gezeri pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:22 Joshua 21:22

na Kibisaumu pamoja na malisho yake, na Beth-horoni pamoja na malisho yake, miji minne.

Yoshua 21:23 Joshua 21:23

Tena katika kabila ya Dani Elteke pamoja na malisho yake, na Gibethoni pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:24 Joshua 21:24

na Aiyaloni pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:25 Joshua 21:25

Tena katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Taanaki pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake; miji miwili.

Yoshua 21:26 Joshua 21:26

Miji yote ya jamaa za wana wa Kohathi waliosalia ilikuwa ni miji kumi, pamoja na malisho yake.

Yoshua 21:27 Joshua 21:27

Tena wana wa Gershoni, katika jamaa za Walawi, waliwapa, katika hiyo nusu ya kabila ya Manase, Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji; na Beeshtera pamoja na malisho yake; miji miwili.

Yoshua 21:28 Joshua 21:28

Tena katika kabila ya Isakari, Kishioni pamoja na malisho yake, na Daberathi pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:29 Joshua 21:29

na Yarmuthi pamoja na malisho yake, na Enganimu pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:30 Joshua 21:30

Tena katika kabila ya Asheri, Mishali pamoja na malisho yake, na Abdoni pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:31 Joshua 21:31

na Helkathi pamoja na malisho yake, na Rehobu pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:32 Joshua 21:32

Tena katika kabila ya Naftali, Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Hamoth-dori pamoja na malisho yake, na Kartani pamoja na malisho yake; miji mitatu.

Yoshua 21:33 Joshua 21:33

Miji yote ya Wagershoni kwa kuandama jamaa zao ilikuwa ni miji kumi na mitatu, pamoja na malisho yake.

Yoshua 21:34 Joshua 21:34

Tena jamaa za wana wa Merari, hao Walawi waliosalia, katika kabila ya Zabuloni, Yokneamu pamoja na malisho yake, na Karta pamoja na malisho yake,

Yoshua 21:35 Joshua 21:35

na Dimna pamoja na malisho yake, na Nahalali pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:36 Joshua 21:36

Tena katika kabila ya Reubeni, Bezeri pamoja na malisho yake, na Yahasa pamoja na malisho yake,

Yoshua 21:37 Joshua 21:37

na Kedemothi pamoja na malisho yake, na Mefaathi pamoja na malisho yake; miji minne.

Yoshua 21:38 Joshua 21:38

Tena katika kabila ya Gadi Ramothi katika Gileadi pamoja na malisho yake, huo mji wa makimbilio kwa ajili ya mwuaji, na Mahanaimu pamoja na malisho yake;

Yoshua 21:39 Joshua 21:39

na Heshboni pamoja na malisho yake, na Yazeri pamoja na malisho yake; jumla yake miji minne.

Yoshua 21:40 Joshua 21:40

Miji hiyo yote ilikuwa ni miji ya wana wa Merari kwa kuandama jamaa zao, ni hizo jamaa za Walawi zilizosalia; na kura yao ilikuwa ni miji kumi na miwili.

Yoshua 21:41 Joshua 21:41

Miji yote ya Walawi iliyokuwa kati ya milki ya wana wa Israeli ilikuwa ni miji arobaini na minane, pamoja na malisho yake.

Yoshua 21:42 Joshua 21:42

Miji hiyo kila mmoja ulikuwa pamoja na malisho yake, yaliyouzunguka pande zote; ndivyo ilivyokuwa katika miji hiyo yote.

Yoshua 21:43 Joshua 21:43

Basi Bwana aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa mumo.

Yoshua 21:44 Joshua 21:44

Kisha Bwana akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye Bwana akawatia adui zao wote mikononi mwao.

Yoshua 21:45 Joshua 21:45

Halikuanguka neno lo lote katika jambo lo lote lililokuwa ni jema ambalo Bwana alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.