Yoshua Mlango 19 Joshua

Yoshua 19:1 Joshua 19:1

Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.

Yoshua 19:2 Joshua 19:2

Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada;

Yoshua 19:3 Joshua 19:3

na Hasarshuali, na Bala, na Esemu;

Yoshua 19:4 Joshua 19:4

na Eltoladi, na Bethuli, na Horma;

Yoshua 19:5 Joshua 19:5

na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa;

Yoshua 19:6 Joshua 19:6

na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;

Yoshua 19:7 Joshua 19:7

na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;

Yoshua 19:8 Joshua 19:8

tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.

Yoshua 19:9 Joshua 19:9

Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

Yoshua 19:10 Joshua 19:10

Kisha kura ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikilia hata Saridi;

Yoshua 19:11 Joshua 19:11

kisha mpaka wao ukakwea kwendelea upande wa magharibi, hata kufikilia Marala, nao ukafikilia hata Dabeshethi; nao ukafikilia kijito cha maji kilicho mkabala wa Yokneamu;

Yoshua 19:12 Joshua 19:12

kisha ukazunguka kutoka Saridi kwendelea upande wa mashariki kwa kuelekea maawio ya jua hata kufikilia mpaka wa Kisiloth-ubori; kisha ukatokea hata Daberathi, kisha ukakwea kwendelea Yafia;

Yoshua 19:13 Joshua 19:13

kutoka hapo ukaendelea kuelekea mashariki mpaka Gath-heferi, hata kufikilia Ethkasini; kisha ukatokea huko Rimoni ufikiliao hata Nea;

Yoshua 19:14 Joshua 19:14

kisha mpaka uliizunguka nchi hiyo kwa upande wa kaskazini hata Hanathoni; kisha matokeo yake yalikuwa katika bonde la Iftaeli;

Yoshua 19:15 Joshua 19:15

na Katathi, na Nahalali, na Shimroni, na Idala, na Bethlehemu; miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:16 Joshua 19:16

Huu ndio urithi wa wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:17 Joshua 19:17

Kisha kura ya nne ilitokea kwa ajili ya Isakari, maana, ni kwa ajili ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao.

Yoshua 19:18 Joshua 19:18

Na mpaka wao ulifikilia Yezreeli, na Kesulothi, na Shunemu;

Yoshua 19:19 Joshua 19:19

na Hafaraimu, na Shioni, na Anaharathi;

Yoshua 19:20 Joshua 19:20

na Rabithu, na Kishioni, na Ebesi;

Yoshua 19:21 Joshua 19:21

na Remethi, na Enganimu, na Enhada, na Bethpasesi;

Yoshua 19:22 Joshua 19:22

na mpaka ukafikilia hata Tabori, na Shahasuma na Bethshemeshi; na matokeo ya mpaka wao yalikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:23 Joshua 19:23

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Isakari kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:24 Joshua 19:24

Kisha kura ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao.

Yoshua 19:25 Joshua 19:25

Na mpaka wao ulikuwa ni Helkathi, na Hali, na Beteni, na Akishafu;

Yoshua 19:26 Joshua 19:26

na Alameleki, na Amadi, na Mishali; nao ukafikilia hata Karmeli upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Shihor-libnathi;

Yoshua 19:27 Joshua 19:27

kisha ukazunguka kuelekea maawio ya jua mpaka Beth-dagoni, nao ukafikilia hata Zabuloni, tena mpaka bonde la Iftaeli upande wa kaskazini hata Bethemeki na Neyeli; kisha ukatokea hata Kabuli upande wa kushoto;

Yoshua 19:28 Joshua 19:28

na Ebroni, na Rehobu, na Hamoni, na Kana, hata kufikilia Sidoni mkuu;

Yoshua 19:29 Joshua 19:29

kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;

Yoshua 19:30 Joshua 19:30

na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:31 Joshua 19:31

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Asheri kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:32 Joshua 19:32

Kisha kura ya sita ikatokea kwa ajili ya wana wa Naftali, maana, ni kwa ajili ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao.

Yoshua 19:33 Joshua 19:33

Na mpaka wao ulikuwa kutoka Helefu, tokea ule mwaloni ulio katika Saananimu, na Adami-nekebu, na Yabineeli, hata kufikilia Lakumu; na matokeo yake yalikuwa katika mto wa Yordani;

Yoshua 19:34 Joshua 19:34

tena mpaka ulizunguka kwendelea upande wa magharibi hata Aznoth-tabori, tena kutoka hapo ukaendelea mpaka Hukoki; kisha ukafikilia hata Zabuloni upande wa kusini, tena ulifikilia hata Asheri upande wa magharibi, tena ulifikilia hata Yuda hapo katika mto wa Yordani kwa upande wa kuelekea maawio ya jua.

Yoshua 19:35 Joshua 19:35

Na miji yenye boma ilikuwa ni hii, Sidimu, na Seri, na Hamathi, na Rakathi, na Kinerethi;

Yoshua 19:36 Joshua 19:36

na Adama, na Rama, na Hazori;

Yoshua 19:37 Joshua 19:37

na Kedeshi, na Edrei, na Enhasori;

Yoshua 19:38 Joshua 19:38

na Ironi, na Migdal-eli, na Horemu, na Bethanathi, na Bethshemeshi; miji kumi na kenda, pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:39 Joshua 19:39

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Naftali kwa kuandama jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:40 Joshua 19:40

Kisha kura ya saba ilitokea kwa ajili ya kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao.

Yoshua 19:41 Joshua 19:41

Na mpaka wa urithi wao ulikuwa ni Sora, na Eshtaoli, na Irishemeshi;

Yoshua 19:42 Joshua 19:42

na Shaalabini, na Aiyaloni, na Ithla;

Yoshua 19:43 Joshua 19:43

na Eloni, na Timna, na Ekroni;

Yoshua 19:44 Joshua 19:44

na Elteka, na Gibethoni, na Baalathi;

Yoshua 19:45 Joshua 19:45

na Yehudi, na Bene-beraki, na Gathrimoni;

Yoshua 19:46 Joshua 19:46

na Meyarkoni, na Rakoni, pamoja na huo mpaka uliokuwa mkabala wa Yafa.

Yoshua 19:47 Joshua 19:47

Kisha mpaka wa wana wa Dani ulitokea kuwapita wao; kwa kuwa hao wana wa Dani wakakwea na kupigana na Leshemu, na kuutwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na kuumiliki, nao wakakaa humo, wakauita Dani, kwa kuliandama jina la huyo Dani mzee wao.

Yoshua 19:48 Joshua 19:48

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Dani kwa kuandama jamaa zao; miji hii pamoja na vijiji vyake.

Yoshua 19:49 Joshua 19:49

Basi wakamaliza hiyo kazi yao ya kuigawanya nchi iwe urithi kwa kuandama mipaka yake; kisha wana wa Israeli wakampa Yoshua, mwana wa Nuni, urithi katikati yao;

Yoshua 19:50 Joshua 19:50

sawasawa na ile amri ya Bwana wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.

Yoshua 19:51 Joshua 19:51

Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya kabila za wana wa Israeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya Bwana, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.