Hunificha Hunificha - Tufani inapovuma

By Elizabeth Nyambura

Lyrics

Tufani inapovuma,
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha,
Mkononi mwa Mungu,

Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.

Pengine kuna taabu,
Yanisongeza kwake,
Najua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.

Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.

Adui wakiniudhi,
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza,
Vyote viwe baraka.

Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.

Niishipo duniani,
Ni tufani daima,
Anilindapo rohoni,
Nitakaa salama.

Hunificha, hunificha, Adui hatanipata
Hunificha, hunificha, Mkononi mwake.

"TUFANI INAPOVUMA BY EVA NYAMBURA"