Nimekubali - Nasema Ndio Bwana

By Eunice Njeri

Lyrics

Nimekubali nasema ndio Bwana 

Kwako ni salama nasema ndio 

Nimekubali nasema ndio Bwana 

Najitoa kwako dhabihu iliyo hai Bwana nitumie


Bwana anatafta watakaomwabudu kwa roho na kweli

Na wakati ndio huu naamini umefika

Nisaidie kutenda kulingana mapenzi yako

Kutembea na maagizo yako moyoni mwangu


Nimekubali nasema ndio Bwana 

Kwako ni salama nasema ndio 

Nimekubali nasema ndio Bwana 

Najitoa kwako dhabihu iliyo hai Bwana nitumie


Mimi ni chombo mikononi mwako Yahweh 

Tena ni udongo na wewe mfinyazi baba, nifinyange nitengeneze

Uishe nafsi yangu chochote utakacho mimi nitatenda


Nimekubali nasema ndio Bwana 

Kwako ni salama nasema ndio 

Nimekubali nasema ndio Bwana 

Najitoa kwako dhabihu iliyo hai Bwana nitumie


Oooh niumbie, niumbie moyo safi, ili niweze kukutukuza

Bwana nitengeneze kwa ajili ya jina lako baba

Wala usinitenganishe na uwepo wako

Mimi bwana eeeh nimekubali njia zako baba

Nasema ndio kwako baba


Nimekubali nasema ndio Bwana 

Kwako ni salama nasema ndio 

Nimekubali nasema ndio Bwana 

Najitoa kwako dhabihu iliyo hai Bwana nitumie


"Eunice Njeri - Nimekubali {OFFICIAL VIDEO}"