Pendo La Ajabu

By Jemimmah Thiong'o

Lyrics

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Pendo ambalo sikupata ulimwenguni


Nilizunguka nikitafuta rafiki

Nukazunguka nikitafuta mpenzi

Rafiki wote walikuwa ni waongo

Naye mpenzi kageuka kuwa hasidi

Waliniacha nikiwa hali mahututi

Niliodhani kuwa ni rafiki zangu

Naye mpenzi akaniharibia sifa

Yesu akaja kwa kweli kaniokoa


Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Pendo ambalo sikupata ulimwenguni


Na kitandani nilikuwa nimelazwa

Marafiki wakanitazama kaenda

Wakasema kweli huyu hawezi pona

Lakini Yesu yeye hakuniacha

Korokoroni kwa kweli mi nilipofungwa

Hakuna aliyetaka kuhusishwa nami

Hakuna ndugu aliyenitembelea

Rafiki Yesu yeye hakuniacha


Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Pendo ambalo sikupata ulimwenguni


Na isitoshe baada ya haya yote

Kanionyesha dhambi zangu huyu mpenzi

Akaniambia nikitubu taniokoa

Niweke huru kisha anipe hai

Niliopata kwa yesu ni ya ajabu

Upendo huu sijapata kuona mwingine

Sasa natangaza wote wakafahamu

Pendo la Yesu ni pendo la ajabu


Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Yesu pendo lako ni pendo la ajabu

Pendo ambalo sikupata ulimwenguni