Nitafika Tu

By Maggie Muliri

Lyrics

Nina imani nitafika 

Jibu ni kufika 

Japo waonekana wasi wasi nitafika niendapo 

Jibu kwa moyo wangu nitafika eeh 

Natamani kuenda kule nionapo 

Nina shauku ya kutekeleza maono yangu eeh 

Lakini vikwazo ni vingi sana aah 

Lakini majaribu ni mengi sana 

Wa kunivunja moyo ni wengi njiani 

Faraoh na Jeshi lake hawataki kuniacha 

Jibu kwa moyo wangu nitafika 

Japo milima na mabonde nitafika 

Nitafika niendapo oooh 

Nahitaji neema yako Jehovah nifike niendapo 

Nahitaji msaada wako Baba nifike niendapo 

Naomba nishike mkono nifike niendapo 

Jibu kwa moyo wangu nitafika 


Bado nina pumzi tumaini langu lipo (nitafika tu) 

Pata leo kesho inakuja ooh (nitafika tu) 

Baada ya kesho mwezi ujao unakuja (nitafika tu) 

Najipa moyo mwaka kesho nitafaulu eeh (nitafika tu)


Hata kama jaribu lako lilikuwa gumu wewe (nitafika tu) 

Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu) 

Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu) 

Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu) 

Ni kufika ni kufika weeee (utafika tu) 

Ni kufika ni kufika weeee (utafika tu) 


Hata usiku uwe mrefu kutakucha 

Hata giza liwe kubwa nuru itatokea 

Jibu la maisha yako ipo leo 

Hata safari iwe na vikwazo utafika 

Hata jaribu liwe nzito utavuka 

Jibu la maisha yako ipo leo 

Unamkumbuka Sarah alipata mtoto uzeeni 

Unamkumbuka Anna mpaka alitengwa oo ooh 

Kumbe tumboni mwake amembeba Samweli 

Neema ya Mungu bado iko nawe 

Yamkini huduma yako imebeba vitu vingi 

Hata akijaliwa kubwa neema nayo ipo 

Neema ya Mungu bado iko nawe 

Hata maji yawe marefu bado kuna ukingo wake 

Neema ya Mungu bado iko nawe 

Huruma ya Mungu bado inakutafuta aah 


Ukaishi sana bila mafanikio ooh (utafika tu) 

Haijalishi shida vikwazo safarini (nitafika tu) 

Sijali wangapi wananikatisha tamaa (nitafika tu) 

Wala sitajali mazingira ninayoyapitia (nitafika tu) 

Hata kama jaribu lako lilikuwa gumu wewe (utafika tu)

Huruma ya Mungu imekutafuta leo (utafika tu) 

Hata kama mapito yalikuwa ni mengi kwako (utafika tu) 

Wema wa Mungu umekutafuta leo (utafika tu) 

Ni kufika ni kufika weeee (utafika tu) 

Ni kufika ni kufika weeee (utafika tu) 

Maggie Muliri Ft Bahati Bukuku - Nitafika Tu (Official Video)