Uheshimiwe Baba - Nikupe Mungu Nini

By Pst. Emmanuel Ushindi

Lyrics

Nikupe Mungu nini?

Nifanye kazi gani?

Wala niseme Neno gani

Nipate Kimbali Mbele Yako

Unitaje Kati Ya Wale Watatu

Unao Jivunia, Washikao Mbedera Yako

Ili Wakuheshimishe, 

Juu Mimi Nimegundua Siri,

Yesu Uko Mali Yangu,

Uko Nguvu Zangu, Na Heshima Yangu

Shuhuda Yako Ni Urithi Wangu

Tena Changamko Ya Moyo Wangu

Ulimwengu muniruhusu Eeeh 

Uhechimiwe Baba


Uheshimiwe Baba, Uheshimiwe Baba 

Uheshimiwe Eeh, uheshimiwe Baba


Heshima yako Baba inayo wivu sana 

Kama vile mwanaume aweka wivu ju ya mke wake 

Ilimshtua Samweli kuona Isreali inaomba mfalme 

Ijapo wana Mungu wa Kweli, Samweli akaogopa 

Alimtuma Nebukadineza, anasukumwa ndani ya mwitu 

Akale majani kama mnyama, sababu alikusahau 

Mfalme moja akalewa, kamata vyombo vya hekalu vitakatidu 

Akavinyeshweya makahaba, kumbe Mungu una wivu 

Message ikatoka mbinguni, ikaandika 

"mene mene tekel upharsin", Ufalme wako umepimwa 

Ona unapewa wengine 

Hasira zako zilitumia Herodi, alipokamata Petro 

akataka mchinga akamuue, akatumia tena kukamata pepo 

Hapo malaika akatoka mbinguni... 

Herodi alipoamka, akakute Petro amekwenda 

Asikari wakashindwa, akasema muandae mkutano 

Aliposema maneno kama mfalme, watu wakapiga mkono 

Wakasema Herode si wewe, lakini sauti yako ni kama Munguu 

Mungu mbinguni akasirika, Herodi tumbo zikatoboka akafa hivo...

Uabudiwe Baba, uabudiwe Baba 

Uabudiwe Baba eeh


Uheshimiwe Baba, Uheshimiwe Baba 

Uheshimiwe Eeh, uheshimiwe Baba 


Najijua kama kabinti, mwanaume hawezi kuniponyoka 

Mabembelenzi ya delila ilimsukuma Samsoni kutoa siri 

Na mimi sitatoka bila Yesu siendi fasi kama siko nawe 

Hata nikilala kitandani nisipokuona Yesu mpaka nitaamuka 

Nitawaambia walinzi wa mji, nitafutieni Yesu mpaka nimshike 

Ahadi zako zanichumbia, maneno yako lasukuma nikupende 

Uko mtamu kwangu unaninogea sana, niende wapi bila wewe? 

Ona mi nalewa sasa, nalewa furaha yako Baba 

Eeeh haleluya ooh haleluya 


Unanilewesha Bwana, unanilewesha sana 

Unanilewesha eeh, Unanilewesha Bwana 


Unanilewesha Bwana, unanilewesha sana 

Unanilewesha eeh, Unanilewesha Bwana


Pastor Emmanuel Ushindi-Uheshimiwe Baba