Maneno

By Rebekah Dawn

Lyrics

Wakati mwingine nikiketi kukuimbia mie 

Huwa nalemewa kupata maneno yanayoshimiri 

Ni kama mtoto mchanga anapojaribu kueleza ukubwa wa sayari 

Ni kama kidege kinapojaribu kueleza upana wa mbingu 

Ni kama changarawe kujaribu kueleza ukubwa wa bahari 

Ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza

Hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu 

Nitatafuta kukuimbia maneno yanayokufaa 

Wakati mwingine nikiketi kukuimbia mie 

Huwa nalemewa kupata maneno yanayoshimiri 

Ni kama tone la maji kujaribu kueleza mfuriko wa mvua 

Ni kama wapendanao kujaribu kueleza fumbo la penzi 

Ni kama mshumaa kujaribu kueleza kung’aa kwa jua 

Ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza 

Hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu 

Nitatafuta kukuimbia

maneno yanayokufaa 

Ni kama jiwe linapojaribu kueleza urefu wa mlima 

Ni kama sheha shupavu kujaribu kueleza hadithi zote za jadi 

Ni kama mwenye dhambi kujaribu kueleza neema ya msamaha 

Ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza 

Hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu 

Nitatafuta kukuimbia, nitatafuta kukuimbia 

Maneno yanaykuofaa 

Maneno - Rebekah Dawn (OFFICIAL MUSIC VIDEO)