Rafiki Pesa

By Shari Martin

Lyrics

Nilikuwa na rafiki yangu

Rafiki Pesa Tulipendana sana

Maisha yetu yalikuwa mazuri

Nitakacho hunipatia


Nikitaka nyumba nzuri alikuwa anijengea

Nikitaka gari nzuri alikuwa aniletea

Nikitaka nguo nzuri anakimbia dukani aniletea

Nikitaka suti nzuri alikuwa aniletea

Nikitaka wanawake anakimbia Florida aniletea

Nikitaka kunywa beer alikuwa aniletea

(Instruments)


Siku moja nilishikwa na ugonjwa mbaya sana

Nikapelekwa kwa madakitari ugonjwa huo haukupona

Waliposhindwa nikarudishwa nchini kwetu nyumbani kwangu

Nikalazwa kitandani kwangu

Nilikuwa naumwa sana


Siku moja Rafiki Pesa akaja kwangu kunitazama

Akaniambia "Rafiki yangu pole sana kwa ugonjwa

Usijali hata ukifa nitakununulia coffin"

Siku ile nilikufa Rafiki Pesa alitoroka

Watoto wangu waliteseka, Majirani waliwacheka

"Pesa alithamini, sasa maisha kwisha"

Utaenda wapi? Utaenda motoni

Wakati urafiki wako na bwana Pesa unapoisha

Mambo mawili anakufanyia

Anakununua kitamba cheupe na coffin ya kukuingiza ndani

Walevi walikunywa pombe wakashindwa na kutembea

Wakitazama chini waona kuna mashimo

Wavuta bangi walivuta sana

Moshi nao ulipoganda

Hata nywele za vichwa zao wakashindwa kuzichana

Matajiri walipata pesa wakazieka kwa anasa

Nazo pesa zaendelea kuwanunulia sanduku


Matajiri walipata pesa wakazieka kwa anasa

Nazo pesa zaendelea kuwanunulia jeneza

Usithamini pesa Pesa zina mwisho, zina mwisho

Pesa zina mwisho Raha nazo baba

Raha zina mwisho, zina mwisho Raha zina mwisho

Shika Yesu baba Yesu ndiye mwisho, ndiye mwisho

Yesu ndiye mwisho Kwa wokovu Baba

Yesu ndiye mwisho, ndiye mwisho

Yesu ndiye mwisho Kwa wokovu Baba

Yesu ndiye mwisho, ndiye mwisho

Yesu ndiye mwisho

03 Shari Martin - Rafiki pesa