Cha kutumaini sina ila damu yake Yesu

By Mbarikiwa

Lyrics

Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha

Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama

Damu yake na sadaka, nategemea daima
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.

Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama

Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga

Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama

Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake

Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama

"Mbarikiwa Cha Kutumainiwa sina NYIMBO ZA TENZI"