Mika Mlango 1 Micah
Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe; Katika Beth-le-Afra ugae-gae mavumbini.
Piteni; uende ukaaye Shafiri, hali ya uchi na aibu; Hivyo akaaye Saanani hajatokea nje; Maombolezo ya Beth-eseli yatawaondolea tegemeo lake;
Maana akaaye Marothi ana utungu wa mema; Kwa kuwa msiba umeshuka toka kwa Bwana, Umefika mpaka lango la Yerusalemu.
Mfungie gari la vita farasi Aliye mwepesi, ukaaye Lakishi; Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni; Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.
Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia; Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.
Bado, ukaaye Maresha, nitakuletea yeye atakayekumiliki; Utukufu wa Israeli utafika mpaka Adulamu.
Jifanyie upaa, jikate nywele zako, Kwa ajili ya watoto waliokufurahisha; Panua upaa wako kama tai; Kwa maana wamekwenda mbali nawe utumwani.