Wimbo Ulio Bora Mlango 2 Song Of Songs
Wimbo Ulio Bora 2:1 SongOfSongs 2:1
Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni.
Wimbo Ulio Bora 2:2 SongOfSongs 2:2
Kama nyinyoro kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti.
Wimbo Ulio Bora 2:3 SongOfSongs 2:3
Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Naliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu.
Wimbo Ulio Bora 2:4 SongOfSongs 2:4
Akanileta mpaka nyumba ya karamu, Na bendera yake juu yangu ni mapenzi.
Wimbo Ulio Bora 2:5 SongOfSongs 2:5
Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi.
Wimbo Ulio Bora 2:6 SongOfSongs 2:6
Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, Nao wa kuume unanikumbatia!
Wimbo Ulio Bora 2:7 SongOfSongs 2:7
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Wimbo Ulio Bora 2:8 SongOfSongs 2:8
Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja, Akiruka milimani, akichachawa vilimani.
Wimbo Ulio Bora 2:9 SongOfSongs 2:9
Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani.
Wimbo Ulio Bora 2:10 SongOfSongs 2:10
Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako,
Wimbo Ulio Bora 2:11 SongOfSongs 2:11
Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake;
Wimbo Ulio Bora 2:12 SongOfSongs 2:12
Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
Wimbo Ulio Bora 2:13 SongOfSongs 2:13
Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.
Wimbo Ulio Bora 2:14 SongOfSongs 2:14
Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za magenge, Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri.
Wimbo Ulio Bora 2:15 SongOfSongs 2:15
Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.
Wimbo Ulio Bora 2:16 SongOfSongs 2:16
Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
Wimbo Ulio Bora 2:17 SongOfSongs 2:17
Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie, Unigeukie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya Betheri.