Wimbo Ulio Bora Mlango 4 Song Of Songs

Wimbo Ulio Bora 4:1 SongOfSongs 4:1

Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua, Nyuma ya barakoa yako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.

Wimbo Ulio Bora 4:2 SongOfSongs 4:2

Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya, Wakipanda kutoka kuoshwa, Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao.

Wimbo Ulio Bora 4:3 SongOfSongs 4:3

Midomo yako ni kama uzi mwekundu, Na kinywa chako ni kizuri; Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako.

Wimbo Ulio Bora 4:4 SongOfSongs 4:4

Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, Uliojengwa pa kuwekea silaha; Ngao elfu zimetungikwa juu yake, Zote ni ngao za mashujaa.

Wimbo Ulio Bora 4:5 SongOfSongs 4:5

Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Nyuma ya barakoa yako. Ambao ni mapacha ya paa; Wakilisha penye nyinyoro.

Wimbo Ulio Bora 4:6 SongOfSongs 4:6

Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie, Nitakwenda kwenye mlima wa manemane, Na kwenye kilima cha ubani.

Wimbo Ulio Bora 4:7 SongOfSongs 4:7

Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila.

Wimbo Ulio Bora 4:8 SongOfSongs 4:8

Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui.

Wimbo Ulio Bora 4:9 SongOfSongs 4:9

Umenishangaza moyo, umbu langu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.

Wimbo Ulio Bora 4:10 SongOfSongs 4:10

Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna.

Wimbo Ulio Bora 4:11 SongOfSongs 4:11

Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali, Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.

Wimbo Ulio Bora 4:12 SongOfSongs 4:12

Bustani iliyofungwa ni umbu langu, bibi arusi, Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri.

Wimbo Ulio Bora 4:13 SongOfSongs 4:13

Machipuko yako ni bustani ya komamanga, Yenye matunda mazuri, hina na nardo,

Wimbo Ulio Bora 4:14 SongOfSongs 4:14

Nardo na zafarani, mchai na mdalasini, Na miti yote iletayo ubani, Manemane na udi, na kolezi kuu zote.

Wimbo Ulio Bora 4:15 SongOfSongs 4:15

Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi.

Wimbo Ulio Bora 4:16 SongOfSongs 4:16

Amka, kaskazi; nawe uje, kusi; Vumeni juu ya bustani yangu, Manukato ya bustani yatokee. Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, Akayale matunda yake mazuri.