Wimbo Ulio Bora Mlango 7 Song Of Songs
Wimbo Ulio Bora 7:1 SongOfSongs 7:1
Siti msharifu, jinsi zilivyo nzuri Hatua zako katika mitalawanda. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, Kazi ya mikono ya fundi mstadi;
Wimbo Ulio Bora 7:2 SongOfSongs 7:2
Kitovu chako ni kama bilauri iliyoviringana, Na isikose divai iliyochanganyika; Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano, Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;
Wimbo Ulio Bora 7:3 SongOfSongs 7:3
Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Ambao ni mapacha ya paa;
Wimbo Ulio Bora 7:4 SongOfSongs 7:4
Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski;
Wimbo Ulio Bora 7:5 SongOfSongs 7:5
Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli, Na nywele za kichwa chako kama urujuani, Mfalme amenaswa na mashungu yake.
Wimbo Ulio Bora 7:6 SongOfSongs 7:6
Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu, Mapenzi katikati ya anasa!
Wimbo Ulio Bora 7:7 SongOfSongs 7:7
Kimo chako kimefanana na mtende, Na maziwa yako na vichala.
Wimbo Ulio Bora 7:8 SongOfSongs 7:8
Nilisema, Nitapanda huo mtende, Na kuyashika makuti yake. Maziwa yako na yawe kama vichala vya mzabibu, Na harufu ya pumzi yako kama mapera;
Wimbo Ulio Bora 7:9 SongOfSongs 7:9
Na kinywa chako kama divai iliyo bora, Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu, Ikitiririka midomoni mwao walalao.
Wimbo Ulio Bora 7:10 SongOfSongs 7:10
Mimi ni wake mpendwa wangu, Na shauku yake ni juu yangu.
Wimbo Ulio Bora 7:11 SongOfSongs 7:11
Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji.
Wimbo Ulio Bora 7:12 SongOfSongs 7:12
Twende mapema hata mashamba ya mizabibu, Tuone kama mzabihu umechanua, Na maua yake yamefunuka; Kama mikomamanga imetoa maua; Huko nitakupa pambaja zangu.
Wimbo Ulio Bora 7:13 SongOfSongs 7:13
Mitunguja hutoa harufu yake; Juu ya milango yetu yako matunda mazuri, Mapya na ya kale, ya kila namna, Niliyokuwekea, mpendwa wangu.