Wimbo Ulio Bora Mlango 1 Song Of Songs
Wimbo Ulio Bora 1:1 SongOfSongs 1:1
Wimbo ulio bora, wa Sulemani.
Wimbo Ulio Bora 1:2 SongOfSongs 1:2
Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai;
Wimbo Ulio Bora 1:3 SongOfSongs 1:3
Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.
Wimbo Ulio Bora 1:4 SongOfSongs 1:4
Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
Wimbo Ulio Bora 1:5 SongOfSongs 1:5
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
Wimbo Ulio Bora 1:6 SongOfSongs 1:6
Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Wimbo Ulio Bora 1:7 SongOfSongs 1:7
Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto, Karibu na makundi ya wenzako?
Wimbo Ulio Bora 1:8 SongOfSongs 1:8
Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji.
Wimbo Ulio Bora 1:9 SongOfSongs 1:9
Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao.
Wimbo Ulio Bora 1:10 SongOfSongs 1:10
Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito.
Wimbo Ulio Bora 1:11 SongOfSongs 1:11
Tutakufanyizia mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
Wimbo Ulio Bora 1:12 SongOfSongs 1:12
Muda mfalme alipoketi juu ya matakia, Nardo yangu ilitoa harufu yake.
Wimbo Ulio Bora 1:13 SongOfSongs 1:13
Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
Wimbo Ulio Bora 1:14 SongOfSongs 1:14
Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
Wimbo Ulio Bora 1:15 SongOfSongs 1:15
Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
Wimbo Ulio Bora 1:16 SongOfSongs 1:16
Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
Wimbo Ulio Bora 1:17 SongOfSongs 1:17
Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi.