Wimbo Ulio Bora Mlango 8 Song Of Songs
Wimbo Ulio Bora 8:1 SongOfSongs 8:1
Laiti ungekuwa kama ndugu yangu, Aliyeyanyonya matiti ya mamangu! Kama ningekukuta huko nje, Ningekubusu, asinidharau mtu.
Wimbo Ulio Bora 8:2 SongOfSongs 8:2
Ningekuongoza nyumbani mwa mamangu, Naye angenifundisha; Ningekunywesha divai iliyokolea,Divai mpya ya mkomamanga wangu.
Wimbo Ulio Bora 8:3 SongOfSongs 8:3
Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu, Nao wa kuume ungenikumbatia.
Wimbo Ulio Bora 8:4 SongOfSongs 8:4
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha, Hata yatakapoona vema?
Wimbo Ulio Bora 8:5 SongOfSongs 8:5
Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Akimtegemea mpendwa wake? Nalikuamsha chini ya huo mpera; Huko mama yako alikuonea utungu, Aliona utungu aliyekuzaa.
Wimbo Ulio Bora 8:6 SongOfSongs 8:6
Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.
Wimbo Ulio Bora 8:7 SongOfSongs 8:7
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa.
Wimbo Ulio Bora 8:8 SongOfSongs 8:8
Kwetu sisi tuna umbu mdogo, Wala hana maziwa; Tumfanyieje umbu letu, Siku atakapoposwa?
Wimbo Ulio Bora 8:9 SongOfSongs 8:9
Kama akiwa tu ukuta, Tumjengee buruji za fedha; Na kama akiwa ni mlango, Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.
Wimbo Ulio Bora 8:10 SongOfSongs 8:10
Mimi nalikuwa ukuta, Na maziwa yangu kama minara; Ndipo nikawa machoni pake Kama mtu aliyeipata amani.
Wimbo Ulio Bora 8:11 SongOfSongs 8:11
Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomi Akawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu; Kila mtu atoe vipande elfu vya fedha kwa matunda yake.
Wimbo Ulio Bora 8:12 SongOfSongs 8:12
Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, li mbele yangu. Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako, Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.
Wimbo Ulio Bora 8:13 SongOfSongs 8:13
Wewe ukaaye bustanini, Hao rafiki huisikiliza sauti yako; Unisikizishe mimi.
Wimbo Ulio Bora 8:14 SongOfSongs 8:14
Ukimbie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya manukato.